Alichonifunza Mama Mboga na Mama Sambua Kuhusu Biashara.
Maisha ni elimu. Kila siku tunayoishi ni nafasi ya kujifunza. Tunajifunza kwa kuona, kusikia na kwa kufanya.
Kujifunza ni kuamua. Mimi niliamua kujifunza katika kila jambo. Kila jambo linalotokea au ninalokutana nalo hujiuliza nini hapa naweza kujifunza. Kujifunza imekuwa ni sehemu ya kila siku katika maisha yangu.
Mwaka huu, mtaani kwangu nilibahatika kuwa na mahusiano mazuri na kinamama wawili wafanyabiashara ndogo ndogo. Mama muuza vitumbua napenda tumwite mama Sambua kama ambavyo mwanangu Jason hupendelea kumuita na Mama muuza mboga, Jason huyu humwita mama Mboga.
Baada ya kuachana naye, nikatafakari ni namna gani dada huyu alivyo na nidhamu ya pesa na malengo. Sikuwahi kuwaza mia mia tulizokuwa tunanunua vitumbua angeweza kufungua genge ndani ya muda mfupi. Ila pia alinifundisha umuhimu wa kukua katika biashara. Nikajiuliza miezi niliyokutana na huyu dada je kwa kiasi gani nimekua. Jibu siri yangu hahhaa.
Siku kadhaa baadaye nikamuona tena mama Sambua anauza vitumbua majumbani. Nikamuuliza kwanini unatembeza tena? Akaniambia kuwa ameona vitumbua vimedorora, wateja hawaendi kule. Nikapata somo jua wateja wako na kwanini wanakuja kwako. Mama Sambua hapa alisahau kwamba thamani ya biashara yake ilikuwa ni kuwapunguzia wateja kasia ya kufuata vitumbua dukani instead wanapata tu majumbani. Nikamkumbuka mentor wangu mmoja anapenda kusisitiza kwamba ujue thamani ya biashara yako (value proposition) nini kinafanya wateja waje kwako.
Mama Sambua hakuishia hapo, sikumuona tena nikaja kukutana naye katika genge lake lililosheheni bidhaa za kutosha. Ila safari hii katika biashara ya vitumbua akaniambia anapikia pale pale hivyo hatembezi tena. I was amazed. Aliamua kubadilisha biashara ila akajua mahitaji ya wateja wa barabarani, wengi huvutiwa na vitumbua vinavyopikwa na sivyo vilivyopikiwa majumbani.
Nilichojifunza kikubwa kutoka kwa mama Sambua ni flexibility na uwezo wake wa kuadapt mazingira bila kupoteza mwelekeo. Ameweza kufungua genge na linakua kwa kasi, ameongeza wateja wapya na kuretain wa zamani ambapo mtu akiamua kufuata bidhaa mahali genge lake lipo ni lazima atanunua vitumbua kama anahitaji. Ila pia alinifundisha umuhimu wa mawasiliano na wateja wako. Kitendo cha kuja kuaga kuwa hatutomuona tena ila anapatikana sehemu fulani kilinisaidia mimi kama mteja kuendelea kuwa mteja wake kwa sababu najihisi ni sehemu ya biashara yake.
Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kama mfanyabiashara definitely nitaenda kutumia tips hizi kutoka kwa mama Sambua na mama Mboga katika kutathmini biashara yangu.
- Je mwaka huu kwa kiasi gani nimekua katika biashara?
- Je nilikuwa na malengo? Kwa kiasi gani nimeweza kuyafikia?
- Kwa upande wa fedha kwa kiasi gani nimeweza kusimamia mapato na matumizi?
- Je nini nimejifunza kutoka kwa wateja wangu?
- Kwa kiasi gani nimetumia nilichojifunza kutoka kwa wateja wangu?
- Je mawasiliano yangu na wateja wangu yako vipi?
Kuna chochote umejifunza kutoka kwa Mama Sambua na Mama Mboga? Karibu kushare.